Uvuvi
Uvuvi
CHAMA CHA MAZINGIRA NA UFUGAJI TIJA TANZANIA(CHAMAUTA) KUPITIA WATAALAMU WAKE TUMEFANYA TAFITI KATIKA SEKITA YA HII YA UVUVI NA KUBAINI KUWA:
Tanzania Ina ukubwa wa Kilomita 942,600 za Mraba na asilimia 6.55 ya eneo Hilo imefunikwa na maji ambayo yanatoa mavuno ya SAMAKI yanayofikia Tani 350,000.
Kiasi hicho kwa kuwa Nchi Ina uwezo wa kuvua Tani 740,000 iwapo Uvuvi utafanyika kwa ufanisi.
CHAMAUTA pia tumebaini kuwa Shughuli za Uvuvi hufanywa na wavuvi wadogo Kwenye Maji baridi na katika ukanda wa bahari ya Hindi ambao huchangia takribani ya asilimia 95 ya Samaki wote wanaodhalishwa nchini.
Hata hivyo Sekita ya Uvuvi Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa pamoja na Uvuvi haramu, zana duni ya uwekezaji mdogo katika sekta hiyo unaosababisha kuvuliwa kwa Samaki wachache.
Chama Cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) kwa kuzingatia Utunzaji wa Mazingira yatakayokabiliana na MABADIRIKO YA TABIA NCHI katika Sekita ya Uvuvi CHAMAUTA tunaamini Kuna njia Bora za Ufugaji wa Samaki utakaozingatia Ufugaji Bora wa Samaki utakaoleta Tija kwa kuzalisha Samaki wengi bila ya kuwa na madhara kwa Mazingira pamoja na Samaki waliyo katika maeneo ya asili kama Bahari, ziwa, na mito ambako wavuvi hurahisisha kazi yao kwa kuvua kwa kutumia baruti au nyavu ndogo ambazo haziruhusiwi na zinachangia kiasi kikubwa Cha uharibifu wa Mazingira.
CHAMAUTA tunahamasisha Ufugaji wa Samaki kweny Vizimba na mabwawa yatakayosaidia kutunza Mazingira na kuleta Tija katika shughuli za Uvuvi.
KUNA FAIDA KUBWA YA KUFUGA SAMAKI KWA VIZIMBA
1. Ufugaji wa Samaki kwa vizimba Unasaidia Samaki kuishi Maisha ya kiasili kuliko kwenye bwawa.
2. Ni Ufugaji wenye Tija unaozingatia Njia za Teknolojia inayozingatia Utunzaji wa Mazingira.
3. Pia Uvunaji wa Samaki wa vizimba ni rahisi kuliko njia zote za Uvuvi.
CHAMAUTA tutakuwa na Vikundi vya wajasiliamali watakaopewa elimu ya ufagaji wa Samaki kwa Vizimba na watapatiwa uwezo na Watalaamu, pamoja na kuviwezesha Vikundi hivyo mitaji ya kufuga Samaki kwa njia hiyo.
Tunafuga Samaki kwa Kuwanenepesha au kuzalisha Vifaranga katika vizimba hivyo.
CHAMAUTA tutajikita zaidi kuvuga Samaki kama vile : SANGARA na SATO ambapo kwa mujibu wa Tafiti ndogo iliyofanywa inaonyesha SANGARA kama atalishwa Samaki wadogo, baada ya miezi 8 Hadi 10. kwa hiyo Ufugaji huo hauto kuwa wa kuzalisha zaidi Vifaranga lakini zaidi utajikita zaidi Kunenepesha Samaki hao. Pia SANGARA ndio Samaki mwenye Soko kubwa Nchi za ulaya.
TATHIMINI UFUGAJI WA SAMAKI KWA VIZIMBA.
CHAMAUTA Tumefanya Tathimini katika kila Kizimba Mfugaji atatarajia kuweka SATO 9000 ambao atawakuza kwa miezi 6 hadi 8. Ambapo Tathimini ya bei ya Soko ni Shilingi elfu 8000 Hadi 10,000 kwa kilo Moja.
