Mazingira

Mazingira

CHAMAUTA TUNAAMINI KUWA MAZINGIRA SALAMA NA
UFUGAJI NI VITU VISIVYOTENGANISHWA. 

  • Mifugo ili iwe salama inategemea mazingira salama yenye uwezo wa
    kuzalisha maji na malisho ya kutosha.
  • Dhana ya utunzaji wa Mazingira na Ufugaji Tija maana yake ni kuendeleza
    mazingira ili mifugo iendelee kuwepo isife kwa ukame wala kukosa Chakula
    na wakati huo huo kutumia njia za kisasa za kuongeza uzalishaji bila
    kutegemea idadi kubwa ya Mifugo au eneo Kubwa la kufugia.
  • Kuendeleza maeneo ya malisho Kwa Kuzalisha malisho, Ili Kuhakikisha Maji
    yanapatikana Kila wakati, Huduma Za Mifugo na Kutumia Mbegu bora zenye
    uzalishaji mkubwa zaidi ni moja ya mikakati ya Chamauta.
  • Kulinda vyanzo vya maji na Kuviboresha kwa Kupanda miti rafiki ya maji ni
    mikakati sahihi ya Kuhakikisha kuwa Mifugo inapata Maji na Malisho Ya
    wakati Wote sasa na Baadae.