Ufugaji

Ufugaji

CHAMA CHA MAZINGIRA NA UFUGAJI TIJA TANZANIA TUNALENGA KUONGEZA TIJA KATIKA UBORA WA MIFUGO.

 “Kwa hiyo, tunahitaji wafugaji wawe na mifugo bora lakini pia yenye tija,” Wafugaji “Wafuge kibiashara pia siyo mtu awe na ng’ombe wengi lakini hawatoi mchango wowote katika uchumi. Uchumi wake binafsi na hata uchumi wake kwa taifa pia.”

CHAMAUTA Tumebaini changamoto kadhaa. Moja wapo ni uhaba wa maeneo ya malisho pamoja na maji kwa ajili ya mifugo. Pia, kuna uhaba wa masoko kwa ajili ya mifugo pamoja na mazao yake.

CHAMAUTA tumebaini Wafugaji wetu nchini kukosa huduma za bima zinazolinda Mifugo hiyo kipindi cha majanga mbalimbali. Halafu, kuna uhaba wa mitaji ya kukuza ufugaji wao. Na bado pia, tuna changamoto ya magonjwa ya mifugo. Halafu kubwa lingine kuendelea na mfumo wa ufugaji usio wa kibiashara.

Kwa hiyo, wafugaji wanapendelea kuwa na Mifugo mingi ambayo haiwapi tija wala kuinua uchumi wao ipasavyo. Tunachangamoto pia ya uhaba na uchakavu wa miundo mbinu. Lakini pia bado tunaona kwa soko la ndani, na hata nje, bado ulaji mdogo wa mazao ya mifugo umekuwa dhahiri. Kwamba watu bado hawatumii maziwa ipasavyo, hawatumii nyama kwa kiwango kinachoshauriwa.

Kwa hiyo, bado tuna changamoto hiyo na matokeo yake sasa tukaona kwamba sambamba na hilo kwamba tunapowahimiza watu kuwa wale nyama, wanywe maziwa, bado uzalishaji uko chini.

Kuna lishe duni kutokana na uhaba wa nyama na maziwa. Na lingine tumeshuhudia dhahiri mabadiliko ya tabianchi. Kwa hiyo, changamoto za ukame, uhaba wa maji ndiyo mambo ambayo tumeyaona kwamba bado ni changamoto kubwa nchini.

Kupitia Changamoto hizo ambazo CHAMAUTA imeziona, Yapo mambo kadhaa ambayo Chama kinaenda kushirikiana na Serikali katika kuongeza Tija.

Moja wapo ni kipengele Cha Mabadiliko ya tabianchi. Kwa hiyo CHAMAUTA, tumezingatia namna ya kushughulika na mabadiliko ya tabianchi kulingana na mazingira tunayo yakabili sasa, na hili ni kutokana na kasumba kuwa Inaaminika kwamba wafugaji wetu ndio chanzo Moja wapo Cha uharibifu wa Mazingira.

Kwa hiyo, tumeangalia namna ya kukuza wigo wa ufugaji, kupata mitaji pamoja na kupata huduma za bima ili kuweza kushawishi uwekezaji zaidi katika maeneo hayo.

Lingine jipya CHAMAUTA tumeweka msisitizo wa uhakika wa chakula na lishe. Kwa hiyo, tunalenga uzalishaji uongezeke zaidi ili watu waweze kupata chakula na lishe ili kupambana na utapiamlo, kupambana na hali ya lishe duni kwa nchi yetu.