TANGAZO LA KUPATA WATAALAM/KAMPUNI WATAKAOSHIRIKI KATIKA MRADI WA SHAMBA LA NG’OMBE WA MAZIWA:
A. UTANGULIZI
CHAMAUTA ni Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania kilichoundwa na
wadau mbalimbali wa utunzaji wa mazingira na ufugaji wenye tija hapa nchini. Wadau
hao ni wale wanaofuga mifugo mbalimbali mfano ng’ombe, kondoo, mbuzi, nguruwe,
samaki, bata, sungura n.k. Hamasa ya kaunzisha chama hiki inatokana na haja ya
kuongeza tija katika ufugaji na kutunza na kuendeleza mazingira ambayo hiyo mifugo
inategemea.
Chamauta katika kutekeleza majukumu yake imekusudia kuanzisha mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wa maziwa utakaojulikana kama CHAMAUTA DIARY FARM PROJECT. Kwa mantiki hiyo Chamauta kinapenda kutangaza nafasi za wataalamu mbalimbali kwaajili ya utekelezaji. Ifuatayo ni orodha ya kazi zitakazohusiana na mradi wetu;
- Uandaaji wa shamba pamoja na ustawishaji wa Miche ya malipo;
- Mfumo wa maji kiujumla pamoja na uchimbaji wa visima na mabwawa;
- Mfumo wa umeme katika eneo la mradi;
- Utunzaji wa mazingira pamoja na upandaji wa miti;
- Ununuzi wa ng’ombe wa maziwa
B. Maeneo yatakayohusika ni kama ifuatavyo;
1) Shamba – hekari 500
2) Maji – hekari 1,000
3) Umeme – hekari 500
4) Mazingira – hekari 60,000
5) Ng’ombe 500
C. Sifa za waombaji
1) Lazima iwe ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania
2) Kampuni iwe na uzoefu wa kazi hizo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu
(3)
3) Kampuni isiwe na tuhuma zozote na hasa ukwepaji wa kodi zozote za Serikali
4) Isiwe inadaiwa na taasisi yoyote ya Serikali au isiyokuwa ya kiserikali
5) Iwe tayari kuonesha au kuthibitisha Uwezo wake wa kifedha
6) Kampuni ioneshe sehemu mbili ambazo imefanya kazi za aina hiyo (yenye
kufanana na mradi mpya) bila hofu.
7) Udhamini wa bank utatokana na majadiliano ya mwisho (final negotiation stage).
8) Kampuni ioneshe orodha ya vitendea kazi inavyomiliki au itakavyokodishiwa au
uthibitisho wa ukodishaji wa vifaa.
D. Maombi yaambatane na vitu vifuatavyo:
- Barua ya Maombi. (Cover letter)
- Wasifu wa kampuni.(CV)
- Muundo wa kampuni. (Company Profile)
“Gharama za kutembelea site ni za muombaji, na ni lazima.
Tarehe itatangazwa baada ya kurudisha fomu za maombi (ofisi itaratibu) na kutakuwa na kikao cha
pamoja (joint meeting) baada ya kutembelea eneo la mradi (site visit)”.
BARUA ZOTE ZIANDIKWE KUPITIA ANUANI HII:
KATIBU MKUU CHAMAUTA,
STENDI KUU GOROFA YA KWANZA,
S.L.P2147,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kupitia barua pepe ya ofisi : info@chamauta.co.tz
Tangazo hili litadumu ndani ya siku 21 za kazi kuanzia leo tarehe 15/03/2024 na mwisho ni tarehe 12/04/2024 saa 11:59 usiku.
